-Nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakutana Bujumbura, Burundi katika kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani pamoja na Kongamano la Kakama.


Na Vero Ignatus

Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kakama) imetangaza maadhmisho ya Siku Kiswahili kuwakutanisha wananchi kutoka mataifa nane ya Afrika Mashariki mjini Bujumbura, Burundi.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili (Kakama), Dk Caroline Asiimwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Julai 5-7 Julai, 2026.

Amesema maadhmisho ya Kiswahili yatatanguliwa na Kongamano la Tatu ka Kakama na kufuatiwa na Siku ya Kiswahiki Duniani Julai 7.

Amesema maadhimisho ya kongamano la Kakama yamkuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili na kutoa fursa kwa kila nchi wanachama.

Amesisitiza kwamba kupitia maadhimisho hayo yamewezesha wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kunufaika na fursa mbalimbali kupitia Kiswahili.

Dk Asiimwe: Kiswahili chafikia hadhi kimataifa kuchangia maendeleo

Aidha lugha ya Kiswahili imetajwa kufikia hadhi ya kimataifa kiwango cha kuwezesha kuwa na mchango wa maendeleo katika nchi wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema lugha ya Kiswahili inaweza kumwezesha mwekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika nchi husika kutokana na kutumika na takribani nchi nane wanachama wa jumuiya.

Dk Asiimwe amesema lugha ya Kiswahili inamwezesha hata mjasiriamali na mfanyabiashara aliyepo kijijini kuamua kuchagua lugha atakayo kupitia akili unde ili kumwezesha kuwasiliana kikamilifu.

Amesema kutokana na maendeleo ya teknolojia, yamewasukuma katika maadhimisho ya Kiswahili Duniani na Kongamano la Tatu yatakayoanyika Bujumbura Julai 5-7 mwaka huu kubeba mjadala wa akili unde na wingi lugha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...