Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata madereva wawili na kuwafungia leseni zao za udereva kufuatia picha mjongeo inayosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikionesha wakiendesha magari kwa njia hatarishi.

Akifafanua tukio hilo leo Juni 01,2026, Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zauda Mohamed amewataja madereva hao kuwa ni Reginald Nzonda aliyekuwa anaendesha gari namba T. 869 EJP na Hatibu Kapire aliyekuwa anaendesha gari namba T. 136 EFP yote aina ya Scania.

Aidha, ametoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani huku akitoa msisitizo kwa madereva vijana wanaokuwa na mihemko ya kutafuta umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupata wafuasi wengi.

Sambamba na hilo amesema kuwa Jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kwa madereva wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Wakizungumza mara baada ya kukamatwa madereva hao, wamesema kuwa walifanya kitendo hicho kwa lengo la kutafuta wafuasi mitandaoni,  ambapo wamejutia kosa hilo ambalo ni kinyume cha sheria na kuwataka madereva wengine kuzingatia sheria wakati wote na kuepuka michezo hatarishi wawapo barabarani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...