Na Pamela Mollel,Arusha

Maonesho ya Kimataifa ya Karibu-KiliFair 2026 yameendelea kuvutia wadau wa sekta ya utalii na ukarimu kutoka ndani na nje ya Tanzania, huku taasisi na kampuni mbalimbali zikitumia jukwaa hilo kutangaza huduma na bidhaa zao kwa soko la kimataifa

Miongoni mwa washiriki wa maonesho hayo ni Masai Safari Lodge Arusha, Masailand Coffee Lodge Karatu pamoja na Tanga Beach Resort, ambazo zimeendelea kuvutia wageni wengi wanaotembelea maonesho hayo kutokana na huduma bora wanazotoa katika sekta ya utalii na ukarimu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkurugenzi wa hoteli hizo, Dkt. Charles Becon, alisema Karibu-KiliFair imeendelea kuwa daraja muhimu la kuwakutanisha wadau wa sekta ya utalii na kuwapa nafasi ya kutangaza huduma zao kwa wateja na washirika wa biashara kutoka mataifa mbalimbali

Alisema ushiriki wao katika maonesho hayo unalenga kuonesha huduma bora zinazotolewa na hoteli hizo pamoja na kuendelea kuitangaza Tanzania kama moja ya maeneo bora ya utalii barani Afrika

"Maonesho haya yanatupa nafasi ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, kujifunza mwenendo wa soko na kutangaza huduma zetu kwa wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani," alisema Dkt. Becon

Aidha, aliwapongeza waandaaji wa Karibu-KiliFair kwa maandalizi mazuri na kiwango kikubwa cha ushiriki wa wadau wa utalii wa ndani na wa kimataifa, jambo ambalo limeendelea kuimarisha hadhi ya maonesho hayo kila mwaka

Dkt. Becon alisema sekta ya utalii inaendelea kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa Tanzania, hivyo wadau wanapaswa kutumia majukwaa kama Karibu-KiliFair kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kuvutia wawekezaji pamoja na watalii zaidi

Aliongeza kuwa Masai Safari Lodge Arusha, Masailand Coffee Lodge Karatu na Tanga Beach Resort zimejikita katika kutoa huduma bora zinazokidhi viwango vya kimataifa, huku zikiendelea kuboresha huduma zake ili kuwapatia wageni uzoefu wa kipekee wanapotembelea Tanzania

Kwa mujibu wa Dkt. Becon, ushirikiano unaojengwa kupitia maonesho hayo utaendelea kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii na kufungua fursa mpya za biashara kwa wadau mbalimbali nchini.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...