KATIKA dunia ya leo ambapo changamoto za maisha zimekuwa sehemu ya kila siku kwa familia nyingi, hatua za kugusa maisha ya watu moja kwa moja zimeendelea kuwa muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Meridianbet imeonyesha hilo kupitia zoezi maalum la ugawaji wa vyakula lililofanyika Buguruni jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeleta matumaini kwa familia nyingi zilizokuwa zinakabiliwa na changamoto za kupata mahitaji muhimu ya kila siku.
Katika tukio hilo lililovutia hisia za wengi, familia zenye uhitaji zilipata msaada wa bidhaa muhimu zinazotumika katika maisha ya kila siku. Miongoni mwa bidhaa zilizotolewa ni mchele, unga, sukari, maharage, mafuta ya kupikia pamoja na vifaa vya usafi wa nyumbani. Msaada huo haukuwa tu wa bidhaa, bali ulikuwa ujumbe wa upendo, mshikamano na kujali hali halisi ya wananchi pamoja na kuchukua hatua za kusaidia pale inapohitajika zaidi.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Corporate Social Responsibility (CSR) wa Meridianbet ambao umekuwa ukilenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet alieleza kuwa kampuni hiyo inaamini kila familia inapaswa kuishi kwa heshima na kupata mahitaji ya msingi bila kukumbwa na njaa. Kauli hiyo iliwagusa wengi waliokuwepo na kuonyesha wazi kuwa Meridianbet haipo tu kwa ajili ya burudani, bali pia kwa ajili ya ustawi wa jamii inayowazunguka.
Wananchi wa eneo la Malapa waliopokea msaada huo walishindwa kuficha furaha yao. Wengi walieleza kuwa msaada huo umefika wakati sahihi ambapo gharama za maisha zimekuwa changamoto kubwa kwa kaya nyingi. Baadhi yao walieleza kuwa bidhaa walizopokea zitasaidia kupunguza mzigo wa matumizi ya familia kwa muda na kuwapa nafasi ya kuelekeza nguvu katika shughuli nyingine za kujipatia kipato.
Mbali na zoezi hili la Buguruni, Meridianbet imeendelea kujijengea heshima kubwa kwa kushiriki miradi mbalimbali ya kijamii inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania. Kuanzia kusaidia watoto yatima, kuchangia sekta ya afya, kuhamasisha elimu kwa vijana, kutunza mazingira hadi kuendeleza michezo na burudani, kampuni hiyo imeonyesha dhamira ya kweli ya kurudisha sehemu ya mafanikio yake kwa jamii.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...