Shule ya Royal Family English Medium Primary School imeendelea kujijengea sifa kubwa baada ya kuibuka kinara kwa kushika nafasi ya kwanza katika Manispaa ya Geita kati ya shule 91 katika mtihani wa Moko ya Kanda ya Ziwa.
Shule hiyo yenye wanafunzi 77 wa darasa la saba walioshiriki mtihani huo wameonyesha kiwango cha juu cha ufaulu ambapo wanafunzi 76 wamepata wastani wa A na mwanafunzi mmoja pekee akipata wastani wa B.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mkurugenzi wa shule Mhandisi Lazaro Philipo amesema mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano mkubwa kati ya walimu, wazazi na wanafunzi.
Ameishukuru jamii kwa kuendelea kuiamini shule hiyo na kuahidi kuongeza juhudi zaidi ili kuifanya Royal Family kuwa kitovu cha elimu bora na maadili mema nchini.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...