Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Serikali ya Tanzania imefafanua uamuzi wake wa kuweka akiba ya fedha za kigeni ikiwemo dola za Marekani na dhahabu, ikieleza kuwa hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya kiuchumi yanayoendelea kuikumba dunia.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, aliyetaka ufafanuzi kuhusu sera ya serikali ya ununuzi na uuzaji wa dhahabu pamoja na maslahi mapana ya taifa.
Dkt. Mwigulu amesema kuwa dhahabu sasa imejumuishwa rasmi katika mfumo wa akiba ya fedha za kigeni, kama ilivyo kwa dola za Marekani, na si bidhaa ya biashara ya kawaida inayotumika kwa matumizi ya kila siku ya kiuchumi.
Amefafanua kuwa mpango wa ununuzi wa dhahabu umeendelea vizuri na hadi sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani tani 27 za dhahabu kama sehemu ya akiba yake ya taifa.
Aidha, Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa dhahabu ya taifa haiuzwi kiholela, na akabainisha kuwa utaratibu wa uuzaji wake, pale inapobidi, hufanywa kupitia taasisi rasmi za fedha au kwa tangazo la umma kupitia magazeti ya serikali, si kwa watu binafsi.
Dkt. Mwigulu amewahakikishia wabunge kuwa hakuna uuzaji holela wa dhahabu unaofanyika, bali mfumo uliowekwa unalenga kulinda maslahi ya taifa na kuimarisha uthabiti wa uchumi wa nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...