Na Mwandishi wetu,
Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali kuhakikisha sanaa na michezo inakuwa sehemu ya ajira na maendeleo kwa Vijana nchini.
Hayo yamebainishwa na Ndugu Emmanuel Shilatu ambaye alikuwa mgeni rasmi kumwakilisha Mkuu wa Wilaya kuzindua mashindano ya Kanda ya Kusini kusaka vipaji vya Sanaa na michezo kwa Watoto.
"Serikali imeweka vipaumbele vyake katika kuendeleza vipawa na vipaji vya Wanafunzi kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Michezo. Hivi karibuni Serikali imeboresha mfumo wa elimu kwa ajili ya kuwaandaa Vijana kujifunza amali mbalimbali zikiwepo za michezo na vipaji mbalimbali vya Sanaa." Alisema Shilatu.
Mwandaaji wa Kambi hiyo ya kusaka vipaji ambao ni Shirika la Compassion International amesema jukwaa hilo ni fursa kwa Watoto na Vijana kuonyesha vipaji vyao na kujijengea mustakabali bora huku wakihaidi ubora, haki, nidhamu na burudani ya hali ya juu.
Mmojawapo wa Mzazi ambaye Mwanae anashiriki mashindano hayo Bi. Prisca Richard alionyesha kufurahishwa na Kambi hiyo ya kusaka vipaji vya Michezo kuwa kipaji cha Mwanae anaona kikienda kukua zaidi na ndoto yake kutimia.
Mashindano hayo yameandaliwa na Shirika la Compassion International ambapo yanafanyika Abbey washiriki wakiwa Watu na timu za kutoka mikoa ya kanda ya Kusini ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 26 Juni 2026 na yatafungwa na Waziri wa Vijana Mhe. Joel Nnauka.



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...