Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB (CRDB Bank Secondary Model School) inayojengwa Upanga katika Halmashauri ya Ilala.
Mheshimiwa Zungu aliyepokelewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa amepongeza kasi ya mkandarasi na kumuomba akamilishe ujenzi mapema iwezekanavyo ili kuwanufaisha wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga.
"Shule hii inajengwa Ilala ila itawahudumia wanafunzi kutoka kila mahali. Nampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela na menejimenti nzima kwa kuona umuhimu wa kujenga shule hii itakayowafaa watoto wa Kitanzania. Nikuombe mkandarasi, ongeza kasi ujenzi ukamilike mapema," amesema Spika Zungu.
Akieleza maendeleo ya mradi huo, Tully amesema utakagharimu jumla ya shilingi bilioni 5. "Itakuwa shule bora na ya kisasa. Tunashukuru serikali ya Manispaa ya Ilala kwa kutuamini na kushirikiana nasi kuboresha maisha ya wananchi," amesema Tully.
Kuhusu kukamilika kwa ujenzi huo, Mhandisi Anna Mafoka, mkandarasi anayeujenga mradi huo amesema mkataba ulitaka shule hoyo ijengwe kwa miezi 10 na kukamilika Machi mwakani lakini watajitahidi majengo yawe tayari kwa matumizi ifikapo Desemba ili Januari yaanze kutumika.


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...