Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU Mkoa wa Geita, imewafikisha mahakamani watumishi wa umma saba kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali zaidi ya Sh milioni 78.

Akizungumza na wanahabari leo Juni 12, 2026, Mkuu wa TAKUKURU Geita amesema watumishi hao walikusanya mapato kupitia mfumo wa LGRCIS kwa kutumia mashine za POS lakini hawakuwasilisha fedha hizo katika akaunti ya Serikali.

"Uchunguzi umebaini watumishi hao walisababisha Serikali kupata hasara ya jumla ya Sh78,875,110/= kinyume na utaratibu," amesema.

Watumishi hao ni: Tatu Jeki Kijungu - Afisa Hesabu Wilaya ya Geita, Sylvanus Ngoya Michael - Mhasibu Wilaya, Ladislaus Katuma Kamhanda - Afisa Mtendaji Kata Nyamalimbe, Melina Damian Buguba - Afisa Uvuvi, Mtani Daniel Yangwe na Allen Michael Kimaro - Makusanya Mapato Manispaa, na Mashalla Charles Nkwande - Afisa Mtendaji Kata Kakubilo.

Baada ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, mashauri 7 yamefunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita leo kwa nambari ECO.13145/2026 hadi ECO.13153/2026.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...