Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umesema umeendelea kutekeleza jukumu lake la kuwaunganisha wananchi na huduma muhimu za kijamii pamoja na fursa za kiuchumi kupitia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na madaraja nchini.
Akizungumza katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa TARURA, Catherine Sungura, alisema lengo kuu la wakala huo ni kuwafungulia wananchi njia za kufikia huduma mbalimbali za kijamii, masoko na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Alisema hadi sasa TARURA imefanikiwa kujenga zaidi ya madaraja ya mawe 400 katika maeneo mbalimbali nchini, hatua iliyochangia kuboresha mawasiliano na usafiri kwa wananchi.
Aidha, Sungura alisema wakala huo umefanikiwa kurejesha kwa zaidi ya asilimia 70 mawasiliano ya barabara katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua za El Nino zilizochangia mafuriko na kusababisha uharibifu wa miundombinu.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo yamewezekana baada ya Serikali kupata ufadhili kutoka Benki ya Dunia, ambao umewezesha utekelezaji wa miradi ya kurejesha miundombinu na mawasiliano ya barabara kutoka ngazi ya vijiji hadi taifa kwa ujumla.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...