Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma Juni 27, 2026, imefanya matembezi ya hisani kutoka ofisi za TRA hadi uwanja wa Kilimani pamoja na bonanza la michezo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya TRA na maandalizi ya kuelekea Tuzo za Mheshimiwa Rais kwa Walipakodi, Julai 1, 2026.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi, amesema TRA imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, ikiwemo kuboresha huduma kwa walipakodi, kuongeza matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa mapato na kuimarisha uhusiano na walipakodi.
Amesema maadhimisho ya miaka 30 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Miaka 30 ya TRA, Kulipa Kodi ni Uzalendo na Ushujaa kwa Maendeleo na Kujitegemea kwa Taifa Letu”, ameongeza kuwa TRA Dodoma kuelekea kilele cha miaka 30 kwa kutekeleza shughuli za uwajibikaji kwa jamii, zikiwemo upandaji miti katika Shule ya Sekondari Miyuji, matembezi ya hisani na bonanza la michezo.
Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Sophia Kizigo, ameipongeza TRA kwa kuendelea kuboresha huduma kwa walipakodi na kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa uadilifu, pia amempongeza Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi, kwa uongozi wake katika kuimarisha mazingira rafiki kwa walipakodi na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato mkoani humo.
Dkt. Kizigo ameeleza ushirikiano unaojengwa kupitia shughuli za kijamii unaongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kuimarisha imani kwa TRA, amewahimiza watumishi wa TRA kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uadilifu, pamoja na walipakodi kuendelea kutimiza wajibu wao kwa maendeleo ya Taifa.
Maadhimisho hayo pia yamehusisha zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kusaidia wanawake wajawazito, watoto na wanaohitaji huduma za dharura pamoja bonanza la michezo lililojumuisha mpira wa miguu, kuvuta kamba,kukimbia ndani ya gunia, kukimbia na yai na kukimbiza kuku, huku matembezi ya hisani yakiwakutanisha watumishi wa TRA na baadhi ya walipakodi kuimarisha mshikamano na ushirikiano.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...