Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amesema wazalishaji, wafanyabiashara na watoa huduma nchini ni nguzo muhimu katika maendeleo ya uchumi kutokana na mchango wao katika uzalishaji, biashara na utoaji wa huduma mbalimbali na jitihada zao zinapaswa kutambuliwa ili kuhamasisha utendaji bora na kuongeza ushindani wenye tija.
Londo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa utambuzi wa kampuni bora 100 za chapa za Afrika zinazotengeneza bidhaa zilizoko barani humo, jijini Dar es Salaam.
Amesema serikali inatambua mchango wa Wafanyabiashara na wazalishaji, na ni njia mojawapo ya kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika shughuli zao za kiuchumi.
"Mwaka huu ni wa kihistoria kutokana na kupitishwa kwa bajeti itakayoweka msingi wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuwa mhimili mkubwa wa ukuaji wa uchumi,hivyo Serikali inaitambua sekta binafsi kama mdau muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Taifa",amesema Londo.
Katika hatua nyingine Mhe. Londo amesema Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara ili kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za uzalishaji, biashara na uchumi wa viwanda, ameeleza kuwa hatua hizo zitasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Kwa upande wake Mratibu wa tuzo hizo, Deogratius Kilawe, amesema kwamba lengo la kuandaliwa kwa tuzo hizo ni kutengeneza ushindani wa soko kwa bidhaa za Afrika, na kuongeza huduma bora kwa wananchi.
“Mwaka wa nne tunawatambua wazalishaji hao sasa, watu walioshiriki kuwania ni takribani 5,000 hadi kufikia mchakato wa kampuni 500, kutoka katika nchi zaidi ya saba,” amesema Kilawe.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...