Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Africa imeanza mwaka wake mpya wa fedha 2026/27 kwa

kishindo. Mapato yamepanda kwa asilimia 31 na kufikia Dola Bilioni 1.853 za Marekani katika robo ya kwanza iliyoishia Juni 30, 2026.


Akizungumza juu ya mafanikio hayo, Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Bw. Sunil Taldar amesema ukuaji huo umechochewa na kasi kubwa ya matumizi ya intaneti na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao - Airtel Money


Faida baada ya kodi pia imepanda kwa asilimia 27 na kufikia Dola Milioni 198. Kwa kuzingatia viwango vya fedha visivyobadilika, mapato yamekua kwa asilimia 21.1.



Ripoti inaonyesha Nigeria ndio iliongoza kwa ukuaji wa asilimia 29.8. Vilevile ukanda wa Afrika ya Kati na Magharibi ya Kifaransa ulikua kwa 18%, wakati Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania imekua kwa asilimia 17.8.


Kwenye upande wa wateja, Airtel sasa ina wateja Milioni 189 baada ya kuongezeka kwa 11.6%. Wateja wa intaneti wamefikia Milioni 87.3 na asilimia 51 ya wateja wote sasa wanatumia simu janja. Matumizi ya data kwa kila mteja pia yamepanda kutoka GB 7.8 hadi GB 10.6 kwa mwezi


Hii inaonyesha Watanzania na Afrika kwa ujumla wameanza kutegemea intaneti na huduma za kifedha za simu zaidi kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...