Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, leo Julai 20, 2026 akiwa mkoani Mbeya amekutana na kusikiliza changamoto, maoni na mapendekezo kutoka kwa makundi mbalimbali ya kijamii.

Makundi yaliyowasilisha hoja zao ni pamoja na wakulima, wafugaji, wachimba madini, wafanyabiashara, wavuvi, mama na baba lishe, machinga, waendesha usafirishaji, mafundi ujenzi, mafundi gereji, wanamichezo, walimu wazalendo, wazee wastaafu pamoja na vikundi mbalimbali vya kijamii.

Ndg. Rabia alipokea kero, ushauri na mapendekezo yaliyowasilishwa na wananchi hao, huku baadhi ya hoja zikijibiwa na nyingine kutolewa maelekezo kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.

Baada ya kikao hicho, Ndg. Rabia aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo endelevu na kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama na yenye utulivu ili wananchi waendelee kufanya shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya taifa.








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...