Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kimesema kimejipanga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuzalisha watumishi wenye weledi kupitia ufundishaji, kufanya tafiti na kuandaa wataalamu watakaosaidia kuharakisha maendeleo ya taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 4, 2026, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Hozen Mayaya, alisema chuo kinaendelea kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi katika taasisi za serikali na sekta binafsi.

Alisema ili kufanikisha Dira ya Taifa 2050 ni lazima taifa liwe na rasilimali watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi, huku akibainisha kuwa asilimia 70 ya mchango katika utekelezaji wa Dira hiyo unatarajiwa kutoka katika sekta binafsi.

Profesa Mayaya alisema chuo kitaendelea kufanya tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa Dira hiyo kwa kutoa suluhisho kwa taasisi mbalimbali.

Aidha, alieleza kuwa chuo bado kinapokea wanafunzi wanaotaka kujiunga na kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada, amebainisha kuwa idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka chini ya 30 wakati wa kuanzishwa kwa chuo hadi zaidi ya elfu 15,000 kwa sasa.

Amesema ongezeko hilo linaonyesha imani ya wananchi kutokana na ubora wa elimu na maboresho ya miundombinu yaliyowekwa na serikali, huku akitumia jukwaa hilo kuwakaribisha wazazi, walezi wa wanafunzi waliohitimu kuweza kuona kuwa ni sehemu sahihi ya kuwapeleka Watoto wao kupata elimu na ujuzi.

Amesema wahitimu wengi wameajiriwa sekta za umma na binafsi, baadhi wamejiajiri  pamoja na kuwaajiri wengine, ambapo kwasasa Makao Makuu ya chuo hicho yapo Jijini Dodoma na Kampasi ndogo ipo Jijini Mwanza huku matarajio Yao nikuongeza Kampasi katika maeneo mengine nchini ikiwemo Daresalam.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...