Na. Mwandishi Wetu, Dar.

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti ameipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa namna ilivyofanya maboresho ya Mitaala ya Elimu nchini yenye lengo la kumfanya muhitimu kuweza kujiajiri au kuajiriwa mara anapomaliza masomo  yake.

Mhe. Magoti ameyasema hayo leo tarehe 12/7/2026 katika maonesho ya Sabasaba ambapo amesema kuwa TET inafanya kazi nzuri ya kuboresha elimu nchini.

"Kwa kweli nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuboresha Elimu nchini hasa hivi karibuni katika maboresho ya mitaala yaliyofanyika, ni tumaini langu kwamba wanafunzi nchi nzima wataendelea kufanya vyema, " Amesema mhe. Magoti.

Pia ameeleza, anafurahia namna wanafunzi wanaendelea kupatiwa vitendea kazi kama vitabu vinavyowapelekea kuendele kufanya vyema wakati wa masomo yao na kuendelea kuipongeza TET kwa uratibu mzuri na upatikanaji wa vitabu  mashuleni.

TET inashiriki katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya  biashara maarufu kama Sabasaba  yaliyoanza tarehe 28, Juni ambapo yanatarajiwa kufungwa hapo kesho, Julai 13.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...