Na George Maziku, Kahama
DIWANI wa Kata ya Majengo, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga Shida Zacharia Soko amechangia chakula chenye thamani ya zaidi ya milioni 6 kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma kwenye shule tatu zilizopo kwenye kata yake.
Chakula hicho amekitoa juzi katika mkutano wa wazazi wa wanafunzi wanaosoma katikà shule tatu za Mama Samia Sekondari, shule ya msingi Anderson Msumba na shule ya msingi Majengo.
Mkutano huo aliuitisha yeye mwenyewe kwa lengo la kuwahasisha wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda.
Diwani huyo alitoa gunia 45 za mahindi yenye thamani ya milioni 2925000, maharage kilogramu 600 zenye thamani ya Sh. milioni 1200000, Mchele kilogramu 600 zenye thamani ya 12000, na sukari kilogramu 600 zenye thamani ya Sh. 1200000.
Akitoa mchanganuo wa mchango huo wakati akiukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya, diwani Soko alisema kila shule itapata gunia 15 za mahindi, kilogramu 200 za maharage, kilogramu 200 za mchele na kilogramu 75 za sukari.
"Mheshimiwa mkuu wetu wa wilaya hapa mbele yako kuna pakeji (package) tatu ya chakula kwa ajili ya watoto wa shule ya sekondari ya Mama Samia, mimi ni mzee wa pakeji tu, hayo ndio mapigo yangu. Pakeji kama hii nimetoa kwa shule mbili za msingi za Anderson Msumba na Majengo", alifafanua Soko.
Akipokea mchango huo, mkuu wa wilaya Nkinda alimpongeza diwani Soko kwa moyo wake wa kujitolea na kumtaka aendelee na moyo huo wa huruma na kujali wanyonge.
"Nakupongeza sana mheshimiwa diwani kwa moyo wako wa kutoa kwa wanyonge, wewe unaweza kufikiri haya unayofanya kuwa mambo madogo lakini nataka nikuambie kuwa haya ni mambo makubwa sana, ninakuomba uendelee na moyo huo na Mungu atakulipa", alisema mkuu wa wilaya Nkinda.
Aliongeza kuwa, " Nami nakuunga mkono kwa kuchangia kilogramu 500 za mahindi ambazo nitazitoa leo hii baada ya zoezi hili la kupokea mchango wako", alibainisha Nkinda.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa wazazi na wadau wengine wa maendeleo kuunga mkono juhudi za diwani Soko kwa kuchangia kwa wingi chakula cha watoto wao wanaosoma katikà shule hizo.
Diwani Soko amekuwa na utaratibu wa kuchangia chakula kwa wanafunzi wanaosoma katika shule tatu za kata yake tangu achaguliwe kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wazazi waliohudhuria mkutano huo waliunga mkono mpango wa kuchangia chakula cha wanafunzi ili kuwasaidia watoto kufuatilia vizuri masomo kutoka kwa walimu wao.
" Ni jambo zuri sana kwasababu itawasaidia watoto wetu kusoma kwa utulivu na kuelewa wanachofundishwa na walimu wao. Mimi nitachangia na ninawashauri wazazi wenzangu kuchangia kwa ajili ya ustawi wa watoto wetu", alisema Zuhura Rashid Salum ambaye ni mzazi wa mwanafunzi anaesoma shule ya msingi Majengo.
Naye Diana James aliyejitambulisha kuwa mzazi wa mwanafunzi anaesoma shule ya msingi Anderson Msumba alikubaliana na Mpango huo na kuahidi kuchangia.
"Mpango huu ni mzuri na muhimu sana kwasababu njaa ni mbaya, mtoto mwenye njaa hawezi kuzingatia kikamilifu masomo yake, hata sisi watu wazima hatuwezi kufanya kazi tukiwa na njaa, Mimi nipo tayari kuchangia chakula kwa mtoto wangu", alisema mzazi huyo.
Magunia 15 ya Mahindi yaliyotolewa na diwani Soko kwaajili ya Chakula katikà shule ya Sekondari Samia iliyopo Kata ya Majengo Manispaa ya kahama
Wazazi Wa wanafunzi Wa shule tatu zilizopo katikà Kata ya Majengo
Diwani Wa kata ya Majengo Zacharia SOKO akifuatilia hotuba ya mkuu Wa wilaya




.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...