Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.), ameshiriki Mhadhara maalum wa kuadhimisha Miaka 51 ya Uhuru wa Muungano wa Visiwa vya Comoro uliofanyika katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mhadhara huo, Mhe. Dkt. Maghembe amesisitiza dhamira ya Tanzania kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu na Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro.
Akizungumza katika mhadhara huo, Mhe. Dkt. Maghembe amesisitiza dhamira ya Tanzania kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu na Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro.
Ameipongeza Serikali na wananchi wa Comoro na kumshukuru Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dr. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih kwa kuandaa tukio hilo muhimu. Aidha, amekumbusha mchango wa Tanzania chini ya uongozi wa Hayati Julius Kambarage Nyerere katika kusaidia harakati za uhuru wa Comoro.
Naye Balozi wa Visiwa vya Comoro Mhe. Fakih aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi zilizopelekea Uhuru wa Comoro mwaka 1975.
Naye Balozi wa Visiwa vya Comoro Mhe. Fakih aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi zilizopelekea Uhuru wa Comoro mwaka 1975.
Alisisitiza kuwa Tanzania imeendelea kuwa mshirika muhimu katika kuimarisha amani, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Nchi hizo mbili zinaendelea kushirikiana kwa karibu katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, ulinzi na usalama, biashara na uwekezaji, uchukuzi, bandari na elimu kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...