Kamati ya Siasa na Utekelezaji ya CCM Mkoa wa Geita imeridhishwa na mwendo wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Jengo hilo lililokwama kwa muda mrefu baada ya mkandarasi kushindwa kumaliza mkataba, sasa linaendelezwa na Halmashauri kupitia force account na limefikia asilimia 68 ya ukamilishaji.
Pesa zilizopokelewa kwa ajili ya mradi huo ni takribani shilingi bilioni 1.8.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila ameipongeza Halmashauri kwa hatua madhubuti zilizochukuliwa kuhuisha mradi huo.
Amesema kwa sasa mwendo wa ujenzi ni wa kuridhisha.
Mwenyekiti Kasendamila amewataka watendaji wa Halmashauri hiyo kuwa tayari kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa viongozi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati bila kusuasua.


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...