Na Pamela Mollel,Arusha
Maelfu ya wananchi jijini Arusha wamepata huduma mbalimbali za afya bila malipo katika kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo jumla ya wananchi 24,871 wamehudumiwa na madaktari bingwa pamoja na wataalamu wa kada mbalimbali za afya
Katika kambi hiyo iliyolenga kuibua changamoto za kiafya mapema na kutoa matibabu kwa wakati, wananchi walipata huduma za uchunguzi, vipimo, matibabu na ushauri wa kitaalamu bila kulipia gharama yoyote
Akizungumza jijini Arusha wakati wa kuhitimisha kambi hiyo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini mapema magonjwa mbalimbali na kuchukua hatua stahiki kabla hali haijawa kubwa
Makonda amesema kuwa upatikanaji wa huduma za afya ni muhimu kwa maendeleo ya jamii, huku akisisitiza wananchi kujiunga na mifumo ya bima ya afya ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu na kupunguza mzigo wa gharama pindi wanapohitaji huduma
Katika kambi hiyo, miongoni mwa mambo yaliyoibua umuhimu wa zoezi hilo ni uchunguzi wa shinikizo la damu ambapo wananchi 6,070 walipimwa, huku watu 1,930 wakibainika kuwa na shinikizo la juu la damu bila kufahamu hali zao
Huduma zilizotolewa zilihusisha maeneo mbalimbali ya afya ikiwemo afya ya mama na mtoto, watoto, macho, masikio, pua na koo, ngozi, afya ya akili, lishe, moyo, figo, damu, mfumo wa mkojo, mfumo wa fahamu pamoja na upasuaji
Kambi hiyo ilihusisha wataalamu 520 wa afya waliokuwa mstari wa mbele kutoa huduma kwa wananchi, huku jumla ya washiriki waliochangia kufanikisha zoezi hilo kutoka kada mbalimbali wakifikia takribani 720
Kwa mujibu wa taarifa za utekelezaji wa kambi hiyo, huduma za afya zilizotolewa zilikuwa na thamani ya karibu Sh250 milioni, hatua inayoonyesha jitihada za kuwafikishia wananchi huduma bora za matibabu bila vikwazo vya gharama
Kambi hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, huku ikitoa fursa kwa jamii kupata uchunguzi wa mapema na elimu kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...