Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) , amesema Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yameonyesha mafanikio makubwa ya sekta ya viwanda na biashara pamoja na fursa zinazotolewa na Serikali kwa vijana na wanawake.

Waziri Kapinga amesema hayo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Waziri Salum, alipotembelea maonesho hayo julai 01, 2026 yanayoshirikisha waoneshaji 3,722 kutoka nchi 23 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai 3 na Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Francisco Chapo, akiwa ameambatana na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, amewataka Watanzania kutembelea maonesho hayo ili kujifunza kuhusu biashara, viwanda na fursa za kuongeza thamani ya mazao.

Amesema bidhaa nyingi zinazozalishwa na wanawake na vijana zinaonesha matokeo ya uwekezaji wa Serikali kupitia mikopo na programu za uwezeshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...