Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, ameendelea na ziara yake ya kata kwa kata ambapo leo ametembelea vijiji vya Mwambao, Weru, Lupalama na Kibebe vilivyopo Kata ya Ulanda, akisikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo.

Akiwa katika Kijiji cha Mwambao, Kiswaga amekabidhi mabati 70 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la watumishi, huku akiwapongeza wananchi kwa kujitolea kushiriki ujenzi huo. Amesema maendeleo ya kweli yanapatikana pale wananchi wanaposhirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Wananchi waliozungumza katika mkutano huo wamepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati, ukarabati wa barabara na upatikanaji wa mnara wa mawasiliano uliorahisisha huduma za mtandao.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...