Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) imesema itaendelea kuimarisha tafiti zinazolenga kuzalisha afua za matibabu zinazozingatia mazingira na vinasaba vya Watanzania, ili kuboresha huduma za matibabu ya magonjwa ya mifupa na mfumo wa fahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, Jijini Dar es Salaam Julai 6, 2026, kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema mara nyingi tiba zinazotumika hutokana na matokeo ya tafiti zilizofanyika katika nchi zilizoendelea pamoja na baadhi ya nchi za bara la Afrika, ambapo afua hizo zinaweza kuwa zimezingatia watu wenye vinasaba tofauti, hivyo wao wameona umuhimu wa kufanya tafiti zitakazozalisha afua zinazokidhi mazingira ya Tanzania.

Aidha, amesema MOI imetimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake na imeendelea kujikita katika maeneo makuu matatu ambayo ni kutoa huduma kwa wagonjwa wa mifumo ya ubongo na mifupa, kufundisha huduma hizo kwa wananchi na wataalam katika ngazi ya shahada ya kwanza, shahada ya pili na ubobezi, pamoja na kufanya tafiti.

Pia amesema taasisi hiyo imeweza kutoa mafunzo kwa wananchi na wataalam kutoka ndani na nje ya Tanzania, hususan katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma za afya katika kanda hiyo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...