Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza, wameaanzisha utafiti wa vinasaba unaolenga kuboresha matibabu ya saratani ya tezi kwa watoto nchini Tanzania na ukanda wa Afrika.

Akieleza kuhusu utafiti huo, Dkt. Advera Ngaiza, Bingwa wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Saratani amesema mradi huo utahusisha uchukuaji wa sampuli za vinasaba na tishu kutoka kwa watoto wenye saratani ya tezi nchini Tanzania. 

Amesema sampuli hizo zitachakatwa katika Maabara Kuu ya MNH, huku uchunguzi wa kina wa kisayansi ukifanyika ili kuelewa kwa nini matibabu ya sasa hayatoi matokeo mazuri kwa watoto wa Kiafrika. 

"Lengo letu ni kugundua dawa salama, sahihi na yenye ufanisi mkubwa zaidi itakayosaidia kutibu saratani ya tezi kwa watoto katika ukanda wa Afrika."

Hatua hii inakuja baada ya kubainika kuwa mifumo mingi ya sasa ya matibabu haitoi matokeo yanayotarajiwa kwa watoto wa ukanda huu wa afrika ikilinganishwa na maeneo mengine duniani. 

Kupitia utafiti huu, watafiti wanatarajia kuweka msingi wa maendeleo ya tiba zinazozingatia tofauti za vinasaba, hatua ambayo inaweza kuleta mapinduzi makubwa katika huduma za matibabu ya saratani kwa watoto barani Afrika.






 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...