WENGE wa Uhuru umewasili wilaya Siha ukitokea Hai mkoani Kilinanjaro ambapo unatarajiwa kukimbizwa kilomita 144 katika wilayani humo na kutembelea miradi ya maendeleo saba.
Akizungumza katika mapokezi hayo, yakiyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Ormelili, Mkuu wa wilaya ya Siha, Christophe Timbuka alisema kuwa, Mwenge huo utazindua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Miradi itakayotembelewa ni uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha afya Ormelili chenye thamani ya milioni 250, uzinduzi wa mradi wa maabara za kemia na fizikia katika shule ya sekondari ya Sikirari wenye thamani ya shilingi milioni 104.71.
Miradi mingine ni kutembelea mradi wa vijana kazi iendelee Lawate wenye thamani ya shilingi milioni 25, uwekaji wa jiwe la msingi daraja la upinde wa mawe Songu (milioni 153.7.), uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa maji Gararagua kwenda vijiji 8 (Bilioni 1.59).
Aidha Mwenge huo utaweka jiwe la msingi mradi wa upanuzi wa shamba la kuku wazazi la Tanbreed (Bilioni 9.71) na kuzindua shule mpya ya sekondari Mitimirefu (milioni 584.28).





.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...