Na Victor Masangu, Kibaha

Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wazazi Taifa Ndg. Fadhili Maganya amewaasa viongozi wa chama cha mapinduzi  (CCM)  ngazi  za Wilaya pamoja na   Mkoa wa Pwani  kuhakikisha kwamba  wanalivalia njuga  suala la kero  ya  migogogoro ya ardhi sambamba na kusikiliza   changamoto mbali mbali   zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya  kikazi yenye lengo la   kukijenga chama pamoja na kukagua uhai wake na kuimarisha jumuiya zake sambamba na kuangalia mwenendo mzima wa utekelezaji wa ilani  ikiwemo kukagua na kutembelea  baadhi ya miradi mbali mbali  ya maendeleo.

Mwenyekiti huyo  amebainisha kuwa katika ziara hiyo pia imelenga kukutana na viongozi mbali mbali wa serikali na kupokea taarifa zao  zinazohusiana  na suala zima la  utekelezaji wa kazi  zao  ambazo wanazifanya katika   maeneo yao  kwenye  nyanja mbali mbali za kimaendeleo.

"Nimeanza ziara yangu ya kikazi katika Wilaya ya Kibaha na lengo kubwa na kwamba ziara hii ni ya kikazi na lengo lake kubwa ni kuangalia uhai wa chama jinsi ilivyo, pamoja na jumuiya zake ikiwa sambamba na kuweza kuangalia na kutembelea miradi mbali mbali ya kimaendeleo na kuzungumza na wanachama," amebainisha Mwenyekiti huyo.

Pia Mwenyekiti huyo   amewasihi  wanachama  na viongozi kuhakikisha kwamba wanaachana  kabisa na tabia ya  kuwasikiliza baadhi ya  wanaharakati ambao  wamekuwa wakibeza mambo mbali mbali ambayo  yanatekelzwa  na serikali ya awamu ya sita  na badala yake  wajikite zaidi katika kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi ambazo anazifanya.

Pia amewahimiza madiwani na   viongozi wengine kuhakikisha wanaweka misingi imara ya  kusimamia  utoaji wa fursa za  mikopo ya asilimia 10  ambayo  inatolewa na halmashauri kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini .

Aidha Mwenyekiti huyo hakusita kumpongeza kwa dhati Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa  kuweza kuchapa kazi  kwa bidii pamoja na kuendelea kutekeleza ilani kwa vitendo katika suala zima la kusimamia fedha ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali  ya maendeleo pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauru ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge akitoa salama zake amesema kwamba Mkoa wa Pwani imeweza kuendelea kutekeleza miradi mbali  mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, umeme, miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa viwanda.

Naye Mjumbe wa halmashauri kuu ya   chama cha mapinduzi (CCM) Taifa   Hamoud Jumaa amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha  chama cha serikali kinaendelea kuwa na mahusiano mazuri ikiwemo sambamba na kutekeleza ilani ya chama.  

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amebainisha kuwa ni jukumu la wanachama kuendelea  na kuweza kushikamana katika kukijenga chama  ikiwa sambamba na kuiimarisha  zaidi kwa vitendo jumuiya zake zote.

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka  amempongeza kwa dhati Mwenyekiti huyo  kwa kuamua kufanya ziara ambayo itaweza kuleta uhai wa chama pamoja na kuimarisha jumuiya zake ikiwa pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka  amempongeza Mwenyekiti wa jumuiya  ya wazazi Taifa kwa kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kuweza kuona umuhimu wa kufanya ziara yake ya kikazi ambayo itaweza kuleta  matokeo chanya katika suala zima la kukiimarisha chama pamoja na jumuiya zake kwa pamoja.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ameanza ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa wa Pwani ambapo ameanza  katika Wilaya ya Kibaha ambapo ameweza kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo katika Zahanati ya Kilimahewa iliyopo kata ya Tangini, Kituo cha afya mlandizi pamoja na  kutembelea mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mlandizi.





                                

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...