Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii, Jeshi la Polisi Wilaya ya Ulanga leo limetembelea Hospitali ya Wilaya ya hiyo na kutoa damu pamoja na vitu mbalimbali kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu hospitalini hapo.

Zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Stephen Chaula, akiwa pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ulanga, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Challe Deogratius ambao waliongoza zoezi la uchangiaji wa damu na kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa na wahitaji waliolazwa hospitalini hapo.

Wakizungumza hospitalini hapo wakati wa shughuli hiyo, kwa pamoja wameupongeza huo Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net) Wilaya ya Ulanga kwa kuratibu zoezi hilo, huku wakibainisha kuwa zoezi hilo haliimarishi tu uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii bali ni tendo lenye thawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Aidha, walieleza kuwa damu iliyochangwa itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo, hususan wajawazito na akina mama waliojifungua, watoto pamoja na wagonjwa wengine wanaokabiliwa na upungufu wa damu.

Jeshi la Polisi limeendelea kuhimiza wananchi na taasisi mbalimbali kushiriki katika shughuli za kujitolea, ikiwemo uchangiaji wa damu, ili kuokoa maisha ya Watanzania na kuimarisha mshikamano wa kijamii.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...