Na Janeth Raphael MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Watanzania wanahitaji amani, usalama na utulivu badala ya vurugu na mivutano ya kisiasa, akisisitiza kuwa mazingira hayo ndiyo msingi wa Serikali kuendelea kutoa huduma bora za kijamii, kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Julai 9, 2026, visiwani Zanzibar wakati wa hafla ya kushuhudia utiaji saini wa Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo.
Amesema maridhiano ya kisiasa hayapaswi kutafsiriwa kama ishara ya udhaifu, bali ni alama ya ukomavu wa kisiasa unaojenga msingi wa umoja, kuheshimiana na ushirikiano miongoni mwa viongozi wenye mitazamo tofauti kwa maslahi ya taifa na wananchi.
Kwa mujibu wa Rais Samia, hatua hiyo inafungua ukurasa mpya wa kuimarisha mshikamano, amani na utulivu nchini, hususan Zanzibar, huku akihimiza siasa kujengwa katika misingi ya hoja, heshima na ustaarabu badala ya chuki, migawanyiko na mivutano isiyo na tija.
Amesema migogoro na siasa za chuki huzuia maendeleo, lakini maridhiano na siasa za staha huweka mazingira bora ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo na kuboresha ustawi wa wananchi.
Rais Samia pia amezitaka pande zote zinazohusika na maridhiano hayo kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa, kuendelea na mazungumzo kwa uwazi na kujenga imani ili kulinda umoja, amani na usalama wa taifa.
Akihitimisha hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kudumisha mshikamano uliojengwa kupitia maridhiano hayo.
"Hekima tuliyoionesha leo ikalindwe kwa matendo mema ya kesho, na imani tuliyoijenga kwa muda mrefu isiangushwe kwa maneno au mienendo isiyo na tija," amesema Rais Samia.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...