Waziri wa Madini, Antony Mavunde ameshangazwa na uwekezaji mkubwa wa bilioni 4.8 uliofanywa na vijana katika kituo cha uchenjuaji wa madini Wilayani Chato.

Ametembelea kituo cha TAMPMED Mining Ltd ambacho kinatoa huduma za kisasa za uongezaji thamani ya madini kwa njia ya CIP na Elution huduma za maabara pamoja na usambazaji wa kemikali za uchimbaji wa dhahabu.

Kwa sasa kituo hicho kina plant 3 zenye uwezo wa kuchakata tani 750 za udongo na shughuli za vat leaching zimeshaanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, *lBw. Ramadhani Tampela amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yenye leseni za kampuni. 

Amesisitiza kuwa kampuni haiwezi kukamilika bila kuwa na maeneo ya uchimbaji.

Kwa upande wake Waziri Mavunde amesema Serikali itaendelea kufuta leseni za watu wasio na nia ili kuwapa fursa wawekezaji wenye nia ya kufanya kazi. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...