Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, Julai 24, akipata maelezo wakati alipotembelea chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) jijini Dar es Salaam leo Julai 24, 2026.


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhakikisha kinakamilisha miradi yote ya maendeleo inayoendelea na kuongeza juhudi za kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kufanya kazi ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu ya usafiri inayotekelezwa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, Julai 24, wakati alipotembelea chuo hicho kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, kwa lengo la kukagua maendeleo ya miradi na kujionea namna serikali ilivyowekeza katika kuimarisha mafunzo ya sekta ya usafiri.

Kihenzile amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya usafiri wa anga, barabara, reli na majini, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na wataalamu wa kutosha watakaosimamia na kuendesha miradi hiyo.

Amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho, ikiwemo majengo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 70 yaliyofadhiliwa na Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuongeza uwezo wa chuo kutoa mafunzo ya kisasa.

"Rai yangu kwa uongozi wa chuo ni kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na muendelee kubuni programu zitakazozalisha wataalamu wa sekta ya anga, majini na ardhini. Hatupaswi kuendelea kutegemea wataalamu kutoka nje wakati tuna vijana wenye uwezo mkubwa," amesema.

Pia amesema miongoni mwa miradi aliyotembelea ni jengo maalumu la mafunzo ya matengenezo ya ndege, jengo la mafunzo kwa wahudumu wa ndege, madarasa ya marubani pamoja na mabweni ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,500.

Aidha, amesema idadi ya wanafunzi chuoni hapo imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 19,000, jambo linaloonesha kukua kwa mahitaji ya wataalamu wa sekta ya usafirishaji nchini.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Ulingeta Obadia Mbamba, amesema ziara ya Naibu Waziri imewapa hamasa ya kuongeza ubunifu na kuhakikisha chuo kinaendelea kuwa kinara katika kuzalisha wataalamu wa sekta ya usafiri.

Amesema Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya usafiri, hivyo chuo kina wajibu wa kuhakikisha kinaandaa wataalamu watakaoweza kuendesha maendeleo hayo na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.

"Naibu Waziri ametusisitiza tusiridhike na mafanikio tuliyofikia, bali tuendelee kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ubora wa mafunzo ili wataalamu wanaohitimu hapa waweze kushindana katika soko la ajira la kimataifa," amesema Mbamba.

Aidha, amesema chuo kitaendelea kutekeleza maelekezo hayo ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sekta ya usafiri, ambayo imeendelea kuwa mhimili muhimu wa kukuza uchumi na utoaji wa huduma nchini.





Matukio mbalimbali katika 
picha za pamoja.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...