-Ni katika mkutano wa kwanza wa mwaka wa ulinzi wa faragha ulioandaliwa na PDPC




Mkurugenzi wa sheria wa Vodacom Tanzania PLC Olaf Mumburi (wa pili kulia), akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa Ulinzi wa Faragha na Taarifa Binafsi, akiwa mmoja wa wazungumzaji katika majadiliano kuhusu ulinzi wa taarifa za kifedha na uchumi wa kidijitali. Mjadala huo uliwahusisha Wakili Dirontsho Mohale kutoka Taasisi ya Baakaedi Profesional Practice (Pty) ltd- Afrika Kusini (kushoto), Mwakilishi kutoka Benki ya Stanbic Tanzania Winston Ishengoma (wa pili kulia), na Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Abdallah Thabiti. Mkutano huo unaendelea jijini Dar es salaam.


Meneja wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Vodacom Tanzania Plc, Upendo Haji (wa nne kushoto), akipokea tuzo ya udhamini kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dk Emmanuel Mkilia (Wa tatu kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango na ushiriki wa Vodacom Tanzania Plc katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyija jijini Dar es Salaam kati ya juni 30 na julai 01 2026. Mbali na kudhamini mkutano huo pia Viongozi wa Vodacom walishiriki katika mijadala mbalimbali iliyolenga kukuza uelewa kuhusu ulinzi wa taarifa binafsi, kuimarisha utunzaji salama wa taarifa, na kukuza ushirikiano kati ya wadau katika kujenga mazingira salama na yenye kuaminika ya uchumi wa kidijitali nchini Tanzania. Wengine ni Mwakilishi…





Mkurugenzi Mtendaji Idara ya Taarifa Binafsi wa Vodacom Group Afrika Kusini, David Smuts (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa mdahalo uliofanyika katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Mdahalo huo ulijadili mada isemayo, “Nafasi ya Kimkakati ya Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) katika Kuimarisha Uwajibikaji wa Taasisi na Kujenga Imani katika Uchumi wa Kidijitali,” ambapo alisisitiza umuhimu wa Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa binafsi katika kuimarisha uwajibikaji wa taasisi, kujenga imani kwa watumiaji wa huduma na kuhakikisha usimamizi wa taarifa unafanyika kwa uwajibikaji katika mazingira yanayozidi kutegemea teknolojia za kidijitali.

Mdahalo huo pia uliwashirikisha Mkuu wa Idara ya Sheria na Faragha katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dkt. Doreen Mwamtangala (kulia); Mkuu wa Uzingatiaji wa Sheria na Utawala wa Benki ya CRDB Plc, Paulo Mwiru (wa pili kulia); na Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Sheria katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Mhandisi Steven Wangwe (kushoto).

Mkuu wa Idara ya Usalama wa Mtandao wa Vodacom Tanzania PLC, Joel Kazoba (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa mdahalo uliofanyika katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo ulijadili mada isemayo, “Je, Ubunifu Unaweza Kustawi Bila Kuhatarisha Faragha?”, ambapo alisisitiza kuwa katika uchumi wa sasa wa kidijitali, ubunifu na ulinzi wa taarifa binafsi vinapaswa kwenda sambamba, huku imani, uwazi na mifumo madhubuti ya ulinzi wa taarifa vikibaki kuwa msingi wa mageuzi endelevu ya kidijitali.

Mdahalo huo pia uliwashirikisha Wakili kutoka taasisi ya Baakedi Professional Practice (Pty) Ltd ya Afrika Kusini, Dirontsho Mohale (kushoto); Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access Tanzania, Imani John (wa pili kulia); na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga (kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...