-Yatwaa tuzo mbili ikiwemo mshindi wa tatu wa jumla

Rais Samia aliambatana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo. Katika hafla hiyo, Vodacom Tanzania ilitunukiwa tuzo mbili ikiwemo Tuzo ya Nafasi ya Tatu katika Kundi la Washindi wa Jumla wa Maonesho hayo na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni kutambua mchango mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo. Tukio hilo lilifanyika Julai 3, 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo wakipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA) walipotembelea banda la Vodacom muda mfupi kabla ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo Julai 3, 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo Vodacom Tanzania ilitunukiwa tuzo mbili, ikiwemo Tuzo ya Nafasi ya Tatu kwa Mshindi wa Jumla wa Maonesho yote na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (kulia), kuhusu huduma ya simu mpya ya smati kitachi inayouzwa na kampuni hiyo ili kuwawezesha Watanzania kuingia katika ulimwengu wa kidijitali wakati Marais hao walipotembelea banda la Vodacom muda mfupi kabla ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA). Katika hafla hiyo, Vodacom Tanzania ilitunukiwa tuzo mbili ikiwemo Tuzo ya Nafasi ya Tatu katika Kundi la Washindi wa Jumla wa Maonesho hayo na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni kutambua mchango mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA), wakifurahia ushindi baada ya kampuni yao kutunukiwa tuzo mbili: Tuzo ya Nafasi ya Tatu kwa Mshindi wa Jumla wa Maonesho yote na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi Julai 3, 2026, na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo, ambaye kabla ya hafla ya ufunguzi aliambatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutembelea banda la Vodacom na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitazama huduma mbalimbali zilizokuwepo ndani ya banda la Vodacom, wakati wa kutembelea banda hilo muda mfupi kabla ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA), baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, kuhusu huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...