Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imetoa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mapambano dhidi biashara haramu ya dawa za kulevya.

Katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo Julai 3,2026 jijini Dar es Salaam mada zilizowasilishwa kwa waandishi walioshiriki mafunzo hayo ni Dawa tiba zenye asili ya kulevya,dawa mpya za kulevya& Maabara Bubu pamoja na Madhara ya Dawa za kulevya

Wakati wa mawasilisho hayo ya mada waandishi pia wameelezwa kwa kina kuhusu sheria zinazohusika na udhibiti wa kemikali bashirifu.

Akitoa mada kuhusu kemikali bashirifu na dawa za kulevya Kamishina Msaidizi Uchunguzi kutoka Mamlaka hiyo Ziliwa Machibya amezitaja sheria  hizo ni Sheria ya kemikali za Viwandani na Majumbani (Udhibiti na Usimamizi) Na. 3 ya Mwaka 2003.

Nyingine ni Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 yaMwaka 2015 (R.E 2020), Vifungu vya (14, 15, 15A) pamoja na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Na. 1 ya Mwaka 2003 marekebisho ya Sheria ya Fedha 2019)

Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Usafirishaji haramu wa Dawa za Kulevya wa mwaka 1988.

Kutokana na sheria hizo pia ametaja kemikamili bashirifu zilizokamatwa maeneo mbalimbali duniani ni Acetone - lita 3360, Ethanol - lita 8750, Azobisisobutyronitrile - kilo 60, Hydrochloric Acid - kilo 1400, Lead acetate - kilo 5000, N-methylformamide-lita 1890.

Dawa nyingine ni Toluene lita 420, Tartaric acid kilo 375, (2-bromoethyl)benzene kilo 13.5, acetic acidi kilo 4.4, Acetone kilo 22.5, benzyl alcohol kilo 434, ethanol kilo 358, hydrochloric acid 1834.36, methylamine 202.5, tartaric acid kilo 21, toluene kilo 67.5

Akitoa mifano ya Uchepushwaji nchini amesema uchunguzi  ulibaini kiasi cha kilo 12 za kemikali bashirifu aina yapseudoephedrine zilikuwa zimechepushwa katika mchakato wa uzalishaji wa dawa za kikohozi na kupelekea uteketezaji wa lita10,000 za dawa zenye pungufu ya kiambata hai cha kemikali hiyo

Pia ukamatwaji wa tani 21.7 za acetic anhydride nchini Pakistani zilizosafirishwa kutoka Tanzania kwa jina bandia la acetic acid

“Mwaka 2025, jumla ya tani 31.76 na lita 183.500 zà kemikali bashirifu zilikamatwa hapa Nchini. Zimezuiliwa kemikali bashirifu tani 734 Kuingia nchini kinyume cha taratibu.

“Kiasi hiki kinahusisha tani 4 za kemikali bashirifu za kutengeneza dawa ya kulevya aina ya fentanaili(kilipangwa kusafirishwa Kwenda Mexico kwa jina bandia la protein biotine) pamoja na kugundulika kwa maabara bubu ya kutengeneza methafetamine mpakani Namanga upande wa Kenya.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...