Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (Mbinga DC) Joseph Rwiza Kashushura, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (Mbinga TC), Amina H. Seif, wametembelea Banda la Mkoa wa Ruvuma katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Julai 7, 2026.
Katika maonesho hayo, wajasiriamali kutoka Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa washiriki waliopata nafasi ya kuonesha bidhaa na huduma zao, hatua inayowapa fursa muhimu ya kutangaza biashara zao, kupata masoko ya uhakika, kuunganisha mitandao ya kibiashara na kujifunza mbinu mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali wengine wanaoshiriki maonesho hayo.
Maonesho ya 50 ya Sabasaba yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji na ubunifu kwa kuwaunganisha wazalishaji, wajasiriamali, wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo ya uchumi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...