Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu wao katika malezi na ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanakua katika mazingira salama yasiyo na vitendo vya ukatili.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Kisiri, ambaye ni Polisi wa Kata ya Ikoma, Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara,alipokuwa akitoa elimu ya Polisi Jamii katika nyumba ya Abwire Thomas hivi karibuni.

Mkaguzi Msaidizi Kisiri amesema wazazi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea, kuwafuatilia na kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zinazoweza kuhatarisha ustawi wao.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya wazazi, jamii na vyombo vya ulinzi na usalama ni muhimu katika kujenga mazingira bora ya malezi na kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...