Watumishi Housing Investments (WHI) imeendelea kuthibitisha ubora wake katika sekta ya makazi baada ya kutwaa Tuzo ya Tatu ya Banda Bora kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), katika kipengele cha Wajenzi wa Makazi (Real Estate Exhibitor).

Ushindi huo unaifanya WHI kuandika rekodi ya kutwaa tuzo katika maonesho hayo kwa miaka mitano mfululizo, jambo linalodhihirisha ubunifu, ubora wa huduma na dhamira ya taasisi hiyo ya kuendelea kutoa suluhisho la makazi bora kwa Watanzania.

WHI imewashukuru wateja, wadau na wananchi wote waliotembelea banda lake katika Maonesho ya Sabasaba, ikiahidi kuendelea kubuni huduma na miradi ya makazi yenye viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kuchangia maendeleo ya sekta ya nyumba nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...