Na Janeth Raphael - Michuzi Tv Bungeni Dodoma
Wakati Bunge limepitisha jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, Mbunge wa Nzega Mjini Hussein BASHE amesema Ndejembi ni kiongozi mwenye uzoefu, nidhamu na uwezo wa kuunganisha watu, huku Watanzania wakihimizwa kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake mapya.
Akizungumza katika kikao cha Mbunge wa Nzega Mjini amesema uteuzi huo wa Ndejembi ni zao la Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye amelelewa ndani ya chama hicho na kufahamu vyema misingi, dhamana na wajibu wa chama kwa Taifa.
Amesema Ndejembi amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu na amelelewa katika misingi ya kuheshimu viongozi na kutekeleza majukumu aliyopewa kwa nidhamu na uaminifu.
“Deo ni zao la Chama Cha Mapinduzi. Ni mtu aliyetokana na CCM na siyo aliyepita tu ndani ya chama. Anafahamu misingi ya chama, dhamana ya chama hiki na wajibu wake kwa Taifa,” amesema.
Aidha, ameeleza kuwa Ndejembi ni miongoni mwa wajumbe wachache ndani ya Baraza Kuu ambao wamekuwa na uwezo wa kuwakutanisha pande zinazotofautiana na kuzifanya zisikilize hoja kwa lengo la kutafuta suluhu.
“Deo ni mjumbe miongoni mwa wachache ambao pande mbili zinapokuwa zinavutana, ana uwezo wa kukutana na pande zote mbili, zikamsikiliza. Anafahamu misingi ya chama na amelelewa kwa misingi ya kuheshimu viongozi na walio juu yake,” amesema.
Kwa upande mwingine, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini vijana waliotokana na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na kuwapa nafasi za kushika dhamana kubwa za uongozi.
Amesema hakuna wasiwasi kuhusu uwezo, tabia, nidhamu na uzoefu wa Ndejembi, akisisitiza kuwa uteuzi huo umefika katika wakati wake.
“Ombi letu ni moja; hatuna wasiwasi juu ya uwezo wake, tabia yake, nidhamu yake na uzoefu wa kujifunza. Ni mvumilivu. Mwenyezi Mungu humuandikia kila mtu kwa wakati wake,” amesema.
Ameongeza kuwa dhamana aliyopewa Ndejembi inakuja katika kipindi ambacho Taifa linahitaji mshikamano, hivyo Watanzania wanapaswa kumpa moyo, kumuombea na kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Amesema Tanzania imepitia changamoto mbalimbali huko nyuma na kwamba ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi, Watanzania wanapaswa kuwa kitu kimoja na kuwaunga mkono viongozi wao.
“Jambo la msingi tumpe ushirikiano. Amepewa dhamana katika nyakati ngumu na ni tofauti na nyakati nyingine zote katika nchi yetu. Anahitaji kupewa moyo, anahitaji kuombewa,” amesema.
Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa Tanzania ni moja na hakuna Taifa jingine kwa Watanzania.
“Taifa letu limetoka kwenye changamoto kubwa sana huko nyuma. Tuna Taifa moja, tuunganeni sote kuwaunga mkono viongozi wetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa letu. Kila nyakati zinapitia changamoto zake na kila nyakati Mungu huwapatia viongozi wake,” amesema.
Amehitimisha kwa kuwataka Watanzania kuwasaidia viongozi waliopo madarakani katika kukabiliana na changamoto za Taifa na kujenga Tanzania yenye umoja, akisisitiza kuwa Mungu amewapa Watanzania viongozi hao kwa wakati huu.
“Tuwaunge mkono viongozi wetu ili tukabiliane na changamoto za Taifa letu na tuweze kujenga Taifa moja, kwa sababu hatuna Tanzania nyingine zaidi ya hii. Leo Tanzania hii Mungu ametupa viongozi hawa,” amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...