Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid (MCC), amewasisitiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kuendelea kulinda amani, utulivu na mshikamano wa Taifa, akieleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kusimamia jitihada za kuboresha na kustawisha maisha ya kila Mtanzania.

Ndugu Rabia amesema kila Mtanzania ni sehemu ya historia na maendeleo ya Tanzania, hivyo ana wajibu wa kulinda amani, umoja na utulivu wa nchi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ametoa kauli hiyo leo, Agosti 23, 2026, wakati akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Pwani yenye lengo la kusikiliza makundi mbalimbali ya kijamii, kubaini changamoto zinazowakabili na kutafuta namna bora ya kuzitatua.

Katika ziara hiyo, Ndugu Rabia amekutana na kuzungumza na makundi mbalimbali, yakiwemo viongozi wa dini, wazee, wakulima, wafugaji, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), umoja wa wasusi, wafanyabiashara, wanamichezo, wavuvi, wanavyuo, walimu, Machinga, Mawinga, Mama Lishe, Baba Lishe, vyama vya ushirika, umoja wa mashamba ya chumvi, wajane, wachimbaji wa madini, maafisa usafirishaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

Amesema CCM itaendelea kusikiliza wananchi na kufuatilia changamoto zao kwa lengo la kuhakikisha jitihada za maendeleo zinagusa makundi mbalimbali na kuboresha maisha ya wananchi.

Ndugu Rabia amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wananchi na Serikali ni muhimu katika kujenga Tanzania yenye amani, umoja na maendeleo endelevu.
















Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...