Na Victor Masangu,Bagamoyo
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga amewahimiza viongozi na wananchi mbali mbali wakiwemo wadau, wanafunzi, walimu,kuhakikisha wanajenga tabia ya kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali kwa lengo la kuweza kujenga afya zao ikiwa pamoja na kuondokana kabisa na changamoto ya kuwa na magonjwa yasiyoambukiza.
Hayo ameyabainisha wakati wa ufunguzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Baobab tangu kuzaliwa kwake ambayo yameweza kushirikisha jumla ya washiriki zaidi ya ya elfu 1000 kutoka maeneo mbali mbali wakiwemo wadau wa michezo, wanafunzi, taasisis wezeshe pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali.
Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa kwa sasa jamii inapaswa kubadilika na kujikita zaidfi katika kufanya mazoezi ambayo yataweza kuwasaidia katika kujenga afya zao na kuondokana kabisa na magonjwa hivyo amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine kuendelea kujitokeza kwa wingi pindi inapojitokeza michezo mbali mbali kama vile mbio za Marathon na michezo mingine.
"Niwapongeze kwa dhjati uongozi wa Baobab kw akuweza kunialika katika sherehe hizi za maadhimisho ya miaka 20 na mimi kama mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo nimewza kushiriki kikamilifu katika mbio za Marathon kwa hiyo kitu kikubwa ninachowaomba wananchi ni kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo ili kuondokana na magonjwa mbali mbali,"amebainisha Mkuu huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi za Shajar Shani Swai ambaye ndio inayoimiliki shule ya Sekondari Baobab amebainisha kwamba lengo kubwa katika Marathon hiyo ni kukusanya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 20 kwa lengo la kuweza kuwasaidia watoto wenye ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu.
"Tunashukuru sisi kama taasisi tumeweza kutimiza miaka 2o tangu kuanzishwa kwake na mimi napenda kusema lengo kubwa ya kufanya marathon hii ni kukusanya zaidi ya milioni 20 ambayo itaweza kusaidia katika kusaidia watoto yatima na wale amabo wanaoishi katika mazingira magumu na tunashukuru tueweza kutimiza malengo yetu,"amebainisha mkurugenzi.
Naye Mwanzilishi wa Taasisi hiyo ya Shajar Sophia Swai amebainisha kwamba wamemua kutumia maadjimisho hayo ya miaka 20 kukusanya fedha hizo ambazo zitaweza kuwasaidia watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja na jamii mbali mbali ambazo zinauhitaji.
Katika maadhimisho hayo ya miaka 20 ya Baobab kumefanyika mbio za kuanzia kilometa 5 hadi kilometa 10 ambapo michezo mbali mbali imefanyika ikiwemo, soka,kikapu, pete,Riadha, kuvuta kamba ambapo washindi wameweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali ya vikombe pamoja na medani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...