Na Janeth Raphael - MichuziTv - Bungeni Dodoma

Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kumwona Deogratius Ndejembi kuwa miongoni mwa viongozi wanaoweza kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa, akielezwa kuwa msaidizi wake mpya katika nafasi ya Makamu wa Rais.

Dkt Mwigulu ametoa pongezi hizo leo Alhamisi, Agosti 27, 2026, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo katika Bunge jijini Dodoma, akianza kwa kumpongeza Ndejembi ambaye amependekezwa kushika nafasi hiyo.

Ndejembi, ambaye ni Mbunge wa Chamwino mkoani Dodoma, alipendekezwa jana Jumatano, Agosti 26, 2026, na vikao vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pendekezo hilo limekuja baada ya Dk Emmanuel Nchimbi kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais, hatua iliyokubaliwa na Rais Samia.

Kabla ya kupewa nafasi hiyo, Ndejembi alikuwa Waziri wa Nishati, nafasi aliyohudumu akisimamia masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati nchini.

Akizungumza Bungeni, Dkt. Mwigulu amemtakia Ndejembi mafanikio katika jukumu hilo jipya, huku akimpongeza Rais Samia kwa kumuamini na kumteua kuwa sehemu muhimu ya uongozi wa Serikali.

Uteuzi wa Ndejembi sasa unafungua ukurasa mpya katika uongozi wa Serikali, huku akitarajiwa kuendelea na majukumu ya kitaifa kwa nafasi yake mpya baada ya taratibu za kikatiba kukamilika.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...