
Maafisa Wakaguzi na Askari wa intake ya 20211/2012 maarufu kwa jina GH Tanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 15 ya utumishi wao kazini katika hafla ambayo itakayofanyika Jumamosi, Agosti 22, 2026, katika Shule ya Msingi Mitindo, Misungwi mkoani Mwanza.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kutathmini safari ya miaka 15 ya utumishi, huku yakilenga kuimarisha mshikamano, upendo na kujitolea katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na jamii kwa ujumla.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi jamii (CP) Alex Mkama, ambaye ataongoza shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika hafla hiyo.
Maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo “THE HEART OF LOVE”, yenye maana ya “MOYO WA UPENDO”, inayosisitiza umuhimu wa upendo, mshikamano, umoja na kujitolea katika utumishi.
Kwa miaka 15, Maafisa Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wamekuwa sehemu ya safari ya utumishi iliyojaa nidhamu, uwajibikaji, uzalendo na kujitoa katika kutekeleza majukumu yao kwa jamii inayolitegemea Jeshi hilo katika ulinzi na mali zao.
Hafla hiyo inatarajiwa pia kutoa fursa ya kuwakumbusha wahudhuriaji umuhimu wa kuendeleza maadili mema ya utumishi, kusaidiana na kuweka mbele maslahi ya jamii.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...