Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, imewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kujitokeza na kuwapeleka watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 kupata chanjo ya matone ya Polio, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Magdalena Dinawi kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, alisema kuwa chanjo ya Polio inayotolewa kwa njia ya matone ni muhimu katika kuzuia ugonjwa wa kupooza unaosababishwa na virusi vya Polio.
Alisema kuwa ugonjwa huo hauna tiba, hivyo kinga kupitia chanjo ndiyo njia muhimu ya kumkinga mtoto dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na Polio.
“Chanjo hii ina umuhimu kwa watoto kwa sababu inazuia ugonjwa wa kupooza ambao kitaalamu tunauita Polio. Ugonjwa wa Polio hauna tiba, ila kinga iliyopo ni kwa kupewa matone ya chanjo ya Polio. Aidha, watoto wanatarajiwa kupata huduma hiyo katika vituo vya kutolea huduma za afya, shule, maeneo ya ibada, masoko, magulio na maeneo mengine ambako watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 wanapatikana,” alisema Dinawi.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha kampeni hiyo inawafikia watoto wengi, wizara imewashirikisha watu maarufu, viongozi wa dini, wazee wa mila na watu mashuhuri katika Jiji la Dodoma ili kusaidia kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto kupata chanjo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Chanjo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Victor Kweka alisema kuwa halmashauri hiyo imelenga kuwafikia jumla ya watoto 207,096 wenye umri wa chini ya miaka 10 katika kampeni hiyo.
Aliongeza kuwa halmashauri imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa chanjo, ikiwemo kutembelea shule zote za awali na msingi pamoja na kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba.
“Tutahakikisha tunapita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha hatuachi mtoto yeyote bila kumpatia chanjo. Tunafahamu kwamba wakati mwingine watoto wanaweza wasiwe shuleni au wasiwe nyumbani,” alisema Kweka.
Aliongeza kuwa timu maalumu zitaelekezwa katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu, ikiwemo masoko na vituo vya mabasi, ili kuwafikia watoto ambao huenda wasipatikane shuleni au nyumbani wakati wa utoaji wa chanjo.
Akizungumza katika semina hiyo ya uhamasishaji, mmoja wa viongozi wa dini, Shekh Ahmed Said alishukuru kwa semina hiyo, akiahidi kushirikiana na viongozi wengine wa dini kuhakikisha ujumbe kuhusu umuhimu wa chanjo unawafikia waumini na jamii kwa ujumla.
Wizara ya Afya na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimeendelea kuwahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutumia fursa hiyo kuwapeleka watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 kupata chanjo ya matone ya Polio ili kuongeza kinga kwa watoto, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...