Waislamu nchini wanatarajiwa kukutana katika Kongamano Kubwa la Haji 2026 litakalofanyika Jumapili ya tarehe 16 katika Ukumbi wa Muhammad Ali jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo linalenga kutoa uelewa kamili kuhusu utekelezaji wa ibada ya Haji, pamoja na kutoa njia mbalimbali za miwezeshano kwa ajili ya waumini wenye kipato cha kawaida ili waweze kutimiza ndoto yao ya kwenda Makka.
Aidha, Idara ya Haji inatarajiwa kutoa mwelekeo mpya kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na Wizara ya Haji ya Saudia yanayohusu usajili, malipo, malazi na huduma za afya. Miongoni mwa wageni walioalikwa ni Sheikh Farah, Sheikh Isa Othman wa London, huku ikitarajiwa Mufti Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir naye atahudhuria.
Katika kongamano hilo pia kutakuwa na maonyesho ya Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za Haji ili wananchi wapate fursa ya kuchagua kwa mujibu wa uwezo wao huku wakiwa wameonya kuepuka waliaghai.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...