Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha

SERIKALI ya Korea Kusini imesema imefurahishwa na maendeleo ya programu ya kuwezesha wanafunzi wa masomo ya ufundi ya Innovative Energy Education Program (IEEP), kupitia chuo cha ufundi Arusha (ATC), ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali yake.

Akizungumza baada ya kutembelea chuo hicho Julai 31 2026, Balozi wa Korea Kusini Nchini Bi. Eunje Ahn amesema Serikali ya Korea Kusini itaendelea ushirikiano na chuo cha ufundi Arusha (ATC), katika fani ya uhandisi wa mitambo na kuhakikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yanatekelezwa.

Balozi Ahn amesema ameridhishwa na ushirikiano uliokuwepo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kupitia chuo hicho cha ufundi na kwamba ufadhili ilioutoa miaka saba iliyopita na kutarajiwa kumalizika mwakani umeleta mafanikio makubwa.

Amesema vijana wengi wa kitanzania wamepata ujuzi na ajira kupitia programu hiyo na kwamba amefurahishwa zaidi na ubunifu ambao umekuwa ukifanywa na vijana hao kwa kubuni teknolojia mbalimbali.

" Chuo kikuu cha Hanyang na Seoul ni miongoni mwa vyuo ambavyo vimekuwa vikishirikiana na chuo hiki cha ufundi Arusha kwa walimu na wanafunzi wake kubadilishana ujuzi, na Leo tumefika hapa ATC kuona maendeleo ya programu tuliyokuwa tukiifadhili  kwa miaka saba kuanzia mwaka 2020 na inaelekea ukingoni kumalizika mwakani2027, nimefurahishwa sana na maendeleo mazuri ya programu hii," amesema.

Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC), Profesa Chacha Mussa amesema Serikali ya Korea imekuwa msaada mkubwa chuoni hapo ambapo imekuwa ikifadhili walimu na wanafunzi wanaosomea kozi ya ufundi.

" Ushirikiano wetu na Korea Kusini kupitia vyuo vikuu viwili vya ufundi nchini huko ulipelekea sisi kuanzisha kozi ya Mechatronics and material engineering, ambayo ni ya kwanza nchini na Afrika Mashariki, ni kozi inayotoa waendesha mitambo kwenye viwanda," amesema.

Amesema kozi hiyo ilianzishwa baada ya serikali ya Tanzania chini ya Hatari Dkt John Pombe Magufuli kuamua kujikita katika kuanzisha viwanda na hivyo chuo hicho kuanza mchakato wa kutayarisha vijana watakaoendesha mitambo viwandani.

" Tulianzisha kozi hii baada ya Serikali kuamua kuanzisha viwanda na hivyo watu wa kuendesha mitambo walihitajika sana, vijana wengi wameshapatikana na wako kazini hivi sasa, yote hii ni Kwa ushirikiano na Serikali ya Korea Kusini ambapo walimu na wanafunzi wanapata fursa ya kushirikiana kimasomo," Amesema.

Mkurugenzi wa kampuni ya I- tech Tanzania na Meneja programu ya Innovative Energy Education (IEEP), inayofadhiliwa na Serikali ya Korea Kusini, Dkt Wob Lee amesema Balozi amefurahishwa na mafanikio ya programu hiyo.

Balozi Ahn ametembelea madarasa, maabara na karakana zinanazotumiwa na wanafunzi wa programu hiyo na kuona bunifu mbalimbali zinazoendelea kufanywa, pamoja na karakana kubwa inayoendelea kujengwa ambayo itatumika Kwa kufundishia pamoja na uzalishaji.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...