-AAHIDI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU, UTII NA UZALENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa dhamana ya kuwa msaidizi namba moja na kuahidi utii, uadilifu, uzalendo na uchapaji kazi.

Makamu wa Rais amesema hayo, wakati akiwasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino, waliojitokeza kumpokea kwa wingi nje ya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais. Amesema ataendelea kufanya kazi ya kumsaidia Mhe. Rais kwa uadilifu na kuwatumikia watanzania wote ili kuharakisha maendeleo.

Aidha Makamu wa Rais amesema ataendelea kuwawakilisha vyema vijana hapa nchini na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inazidi kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Akitoa salamu zake kwa wananchi hao, Makamu wa Rais amewahakikishia kuendelea kutekeleza majukumu yake mapya kwa uadilifu, bidii na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

“Wana sitawazingua, na Mama sitamzingua,” amesema Ndejembi, katika ujumbe uliosisitiza dhamira yake ya kutekeleza wajibu aliopewa na kuendelea kuwa mwaminifu na mwakilishi mwema wa vijana.

Makamu wa Rais amewasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino ikiwa ni
jimbo alilolitumikia kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...