Farida Mangube Morogoro 

Serikali imewataka watanzania   kuitumia vizuri fursa  ya Tanzania kuwa mwenyeji  wa  mashindano ya AFCON 2027 kwa kutangaza   tamaduni za makabila mbalimbali  kama sehemu ya vivitio adimu vinavyopatikananchini humo  sambamba na  kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.

Kauli hiyo Imetolewa na  Mkuu wa Mkoa  Morogoro,Adam Malima  wakati akifungua Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika mjini Morogoro  ambapo jumla ya wahiriki 150,000 kutoka mikoa mbalimbali wanaonyesha  tamaduni.zao.

Amesema katika michuano hiyo  licha ya Tanzania kushiriki nchi zingine ni Kenya na Uganda ambazo  zinaendelea na maandalizi ya michezo  hiyo ambapo kwa Tanzania itafanyika Arusha,Dar es salaam na Zanzibar.

Aidha amewataka watanzania kuendelea kuheshimu utamadani kwani bila kuwepo Kwa  utamaduni huwezi kuwa na  heshima.

Naye  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema tamasha Hilo la Kitaifa la Utamaduni lilianzia Mkoani Dar Salaam,likaenda Songwe na Ruvuma na Mwaka huu linafanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumzia kuhusu  michuano ya AFCON  Msigwa amewataka watanzania watanzania  kuachiana  maneno yanaenezwa na baadhi ya watu wasioitakia mema   kwa kueneza uongo kuwa  michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mwakani kwa nchi tatu za Tanzania,Kenya na Uganda kuwa Kwa Tanzania imehamishwa sio taarifa za kweli.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...