Na Janeth Raphael – MichuziTv - Bungeni Dodoma
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema matumizi bora na sahihi ya ardhi ni msingi muhimu wa kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini, huku akisisitiza kuwa Serikali haitawafumbia macho wanaokiuka sheria kwa kuingiza mifugo katika mashamba ya wananchi.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Agosti 26, 2026, bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, aliyetaka Serikali kueleza hatua zinazochukuliwa kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo katika baadhi ya maeneo imekuwa ikisababisha vifo na uharibifu wa mali.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema migogoro hiyo bado ni changamoto katika maeneo mbalimbali nchini, lakini utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi unaweza kuwa njia muhimu ya kupunguza na hatimaye kuimaliza.
Amesema sehemu kubwa ya migogoro hiyo inachangiwa na kutokuzingatiwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi, hali inayosababisha wakulima na wafugaji kuingia katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa ajili ya shughuli zao.
“Nimpongeze mbunge kwa swali lake. Mimi kabla ya kuwa katika nafasi hii niliwahi kuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo na wakati ule nilishuhudia vifo vya ng’ombe 150, lakini mkulima akapigwa mkuki. Kwa hiyo najua hali ilivyo katika baadhi ya maeneo mengine,” alisema Dkt. Mwigulu.
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia ukiukwaji wa sheria unaofanywa kwa makusudi, akiwamo mtu anayechukua mifugo na kuiingiza katika mashamba ya wananchi.
“Watu ambao wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuingiza mifugo kwenye mashamba ya watu, hili ni suala la kisheria na sisi kama Serikali hatutalifumbia macho kabisa. Niwaombe Watanzania kuzingatia sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi,” alisema.
Aidha, Dkt. Mwigulu ameziagiza wizara zinazohusika na sekta za kilimo na mifugo kushirikiana kwa karibu katika kuweka mifumo na mazingira yatakayosaidia kuzuia na kuondoa migogoro hiyo.
Amesema katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa mabwawa na miradi ya umwagiliaji, ni muhimu Serikali kuhakikisha maeneo maalumu yanatengwa kwa ajili ya wafugaji na mifugo yao ili kuepusha mwingiliano wa shughuli hizo na maeneo ya kilimo.
“Lazima tufanye transform kupitia wizara zetu. Kama kuna ujenzi wa bwawa na kilimo cha umwagiliaji, basi kuwepo na maeneo maalumu kwa ajili ya wafugaji na mifugo yao ili kuondoa migogoro hii,” amesema.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, wakulima na wafugaji, pamoja na kuzingatia sheria na mipango ya matumizi ya ardhi, ni muhimu katika kumaliza migogoro hiyo, kulinda maisha ya wananchi na kuhakikisha mali zao zinakuwa salama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...