Na Janeth Raphael – MichuziTv
Mwalimu wa Shule ya Awali DCT Canon Andrea Mwaka, Rose Isaka, aliyewahi kumfundisha Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, mwaka 1986, amemuelezea kiongozi huyo kuwa tangu akiwa mtoto alikuwa na tabia ya furaha, ucheshi, upole na kujali watu waliomzunguka.
Akizungumza kuhusu kumbukumbu zake za kipindi hicho, Rose amesema Ndejembi alikuwa mwanafunzi mwenye nidhamu na tabia njema, aliyependa kushirikiana na wenzake pamoja na kushiriki katika michezo, hususan mpira wa miguu.
“Alikuwa mwanafunzi mzuri sana, mcheshi na mwenye furaha wakati wote. Nimefurahi sana kwa sababu alikuwa ni mwanafunzi wangu,” amesema.
Amesema moja ya matukio ambayo yameendelea kubaki kwenye kumbukumbu yake ni pale Ndejembi alipomsaidia mwanafunzi mwenzake aliyeanguka na kuumia wakati wa michezo.
Kwa mujibu wa Rose, baada ya kuona mwanafunzi huyo ameumia, Ndejembi alimfuata na kumsaidia, jambo ambalo aliliona kama ishara ya kujali na kuwathamini wenzake tangu akiwa katika umri mdogo.
“Alikuwa hana matukio mabaya ya kutisha, hapana. Tukio ninalolikumbuka ni siku ambayo mwanafunzi mwenzake alianguka na kuumia, Ndejembi akaenda kumsaidia na kumhudumia vizuri sana. Hicho ndicho ninachokumbuka mpaka leo,” amesema.
Rose amesema tukio hilo lilimfanya kumtambua Ndejembi kama mtoto mwenye moyo wa kuwajali wengine, akieleza kuwa hulka ya kusaidia na kushirikiana na watu ilionekana wazi tangu utotoni.
Amesema anaamini tabia hizo njema alizokuwa nazo akiwa mtoto zimeendelea kuwa sehemu ya maisha yake hadi sasa, huku akimtakia mafanikio na kumwombea aendelee kuwa kiongozi mwenye moyo wa kuwasaidia wengine.
“Ninamwombea baraka kibao. Ninamwombea kwa Mungu aendelee kuwa mwema. Mungu azidi kumbariki sana na aendelee na tabia yake ileile ya kusaidia watu wote kama alivyokuwa utotoni,” amesema Rose.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...