Na Victor Masangu, Kibaha

Katika kupambana na wimbi la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi kwa wanawake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja ameamua kutoa darasa maalumu kwa ajili ya kufundisha mafunzo ya ujasiriamali na jinsi ya kutenghheneza bidhaa kwa wanawake mbali mbali kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuachana na kuwa tegemezi ikiwa sambamba na kujikwamua kiuchumi

Hayo yamebaishwa wakati wa ziara yake maalumu yenye lengo la kuweza kukutana na baadhi ya makundi ya wanawake kwa ajili ya kutoa darasa la mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali yenye lengo la kuwaongozea ujuzi na elimu ambayo itawasaidia katika kutengeneza biadha za aina tofauti.

Mwenyekiti huyo ametoa darasa la mafunzo hayo kwa wanawake wa jumuiya ya UWT katika kata mbili za Msangani na Kata ya Mkuza ambapo zaidi ya wanawake 100 wameweza kupatiwa mafunzo mbali mbali ya kutengeneza bidhaa mbali mbali ikiwemo kufundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa za batiki, sabuni za kuogea, sabuni za chooni,shampuu kwa ajili ya nywele.

Mgonja amebainisha kwamba ametoa kutoa elimu hiyo ya darasa la mafunzo ya ujasiriamali bure bila malipo ikiwa ni utekelezaji wake wa ahadi ambayo aliitoa wakati akiwa katika ziara yake ya kuwashukuru wanawake hao ambao waliweza kukiheshimisha chama wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo waliweza kupiga kura za kisdindo.

"Ahadi ni deni kwa hiyo mimi kama Mwenyekiti wa UWT nimekuja kuwapa elimu na mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali bila malipo ya iana yoyote na kwamba mafunzo hayo ni moja ya ahadi yangu ambayo niliitoa wakati nikiwa katika ziara yangu ya kutoa shukrani kwa wanawake kukipigia chama cha mapinduzi kura nyingi za kishindo katika uchaguzi mkuu,"amebainisha Mwenyekiti Mgonja.

Kwa upande wake Katibu katibu wa UWT Cesilia Ndaru amewahimiza wanawake kuhakikisha kwamba wanatumia fursa mbali mbali za ujasiriamali na kuachana kabisa na tabia ya kuwa na majungu na kuzungumza maneno ambayo hayana faida yoyote na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali.

Naye mjumbe wa kamati ya utekeelzaji wa UWT Zainabu Gama amebainisha kwamba darasa la mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wanawake hao katika kujiongezea kipato na kujikwamu kiuchumi.

Nao baadhi ya wanawake kutoka kata za Msangani na Mkuza ambao wameweza kupata fursa ya kupata elimu hiyo ya kutengeneza bidhaa mbali mbali wamesema wamempongeza Mwenyekiti wa UWT kwa kuwapatia darasa hilo la elimu ambayo itakwenda kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua na wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi.

Ziara maalumu ya Mwenyekiti wa UWT Kibaha mjini ambayo imendaliwa mahususi kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake ambayo aliitoa ya kuwa na darasa la kutoa elimu ya ujasiriamali na jinsi ya kutengeneza bidha bila malipo ambapo ameanza mafunzo hayo katika kata mbili za Msangani pamoja na Mkuza.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...