MWANAFUNZI wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Ufundi Tanga, Neema Bundala akionesha uwezo wake wa kujua mfumo wa nchini unafavyofanya kazi kwenye Banda la NACTVET ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika  katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
MWANAFUNZI wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Ufundi Tanga, Neema Bundala, amesema mkondo wa Amali katika shule za sekondari unawajengea wanafunzi ujuzi unaowawezesha kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo, huku wakisubiri matokeo ya mitihani ya Taifa.

Neema ameyasema hayo wakati akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika Banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga

Amesema anasoma fani ya Ufundi wa Magari (Motor Vehicle Mechanics), ambapo mafunzo hayo yanamwezesha kupata ujuzi wa vitendo utakaomsaidia kuanza kujiajiri mara baada ya kuhitimu.

“Kwa mfano mimi nasoma Ufundi wa Magari, hivyo ninapohitimu nitakuwa na ujuzi wa kutengeneza magari na ninaweza kuanza kujiajiri na nikisoma Kidato cha Tano na cha Sita, nitakuwa nimeongeza umahiri na nikifika chuo nitakuwa mbobezi zaidi,” amesema Neema.

Amesema mkondo wa Amali ni muhimu kwa wanafunzi wa kike kwa kuwa unawapa fursa ya kujenga uwezo wa kujiajiri na pia kuajirika katika taasisi mbalimbali kutokana na kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...